HabariNews

Zaidi ya familia 10 Diani zakabiliwa na tishio la kufurushwa kutoka kwenye nyumba zao…..

Zaidi ya familia 10 katika eneo la Diani kaunti ya Kwale sasa zinakabiliwa na tishio la kufurushwa kutoka kwenye nyumba zao na bwenyenye mmoja baada ya mahakama kuidhinisha kubomolewa kwa nyumba zao.

Wakizungumza na wanahabari, wenyeji hao wanasema kuwa ardhi yao inayokabiliwa na utata ni shamba la ekari 6, swala ambalo wanasema linawahangaisha sana kwani hawana pahali pakwenda ikizingatiwa kuwa hapo ndio nyumbani kwao.

Wakaazi hao wameitaka serikali ya kaunti ya kwale kuingilia kati na kusaidia kutatua mzozo huo haraka iwezekanvyo kwani tishio la kunyakuliwa kwa ardhi yao linawakera mno.

BY NEWS DESK