HabariNews

Wakaazi wa Kilibasi katika eneo bunge la Kinango kaunti ya Kwale wameitaka serikali ya kitaifa na ile ya kaunti kuwasaidia kutokana na makali ya janga la ukame.

Wakaazi wa Kilibasi katika eneo bunge la Kinango kaunti ya Kwale wameitaka serikali ya kitaifa na ile ya kaunti kuwasaidia kutokana na makali ya janga la ukame.

Wakiongozwa na Eunice Wanza, wamedai kuwa janga hilo limechangia kuathirika kwa shughuli za biashara ya makaa wanazozitegemea kimaisha.

Wakaazi hao sasa wanaitaka serikali kutoa misaada ya chakula na maji baada ya ukame unaoshuhudiwa katika eneo hilo kuwaathiri hasa wanawake na watoto.

Kwa upande wake mwakilishi wa wadi ya Puma James Dawa amesema kuwa tayari wamewasilisha mswada unaolenga kushughulikia suala hilo bungeni.

Dawa ameeleza kwamba mswada huo unalenga kuishinikiza serikali ya kaunti kutenga fedha za kuwasaidia waathiriwa.

BY NEWS DESK