HabariNewsSiasa

Jaji mkuu Martha Koome anatarajiwa hapo kesho kuzindua rasmi maono yake kwa idara ya mahakama….

jaji mkuu Martha Koome anatarajiwa hapo kesho kuzindua rasmi maono yake kwa idara ya mahakama kwenye majengo ya mahakama ya juu.

Uzinduzi huo unatarajiwa wiki moja tu baada ya Koome kukamilisha siku 100 ofisini tangu kuanza kuhudumu kama jaji mkuu na mwanamke wa kwanza kushikilia afisi hiyo.

Maono yake yanalenga kuleta mageuzi kwenye masuala ya kijamii kupitia kupatikana kwa haki kwa wote.

Akizungumza wakti wa hafla ya maadhimisho ya siku 100 ofisini, Koome alisema kuwa malengo yake ni kuhakikisha idara ya mahakama ihuru, yenye ufanisi ya kuwapa wakenya haki kwa urahisi na yenye uwajibikaji.

BY JOYCE MWENDWA