HabariNews

Serikali ya Kilifi yazindua miradi mitatu ya kusambaza maji huko Magarini…..

Serikali ya kaunti ya kilifi imezindua miradi mitatu ya usambazaji maji kwa gharama ya shillingi millioni 20 katika eneo bunge la Magarini.

Miradi hiyo ni pamoja na ule wa Masheheni, Mbaoni na Mwangatini ulio gharimu Shillingi millioni 12 na itafikia watu 3,500 pamoja na ule wa Misufini Baungo  uliogharimu shillingi millioni nne na utahudimia watu 1,500 na mwengine wa Marekebuni Bomani iliogharimu shillingi millioni 4 ambao ulifikia watu 1800.

Mradi huo ulizinduliwa rasmi na gavana wa Kilifi Amason Kingi pamoja na naibu wake Gideon Saburi na utapunguza umbali wa wakaazi kutafuta maji kutoka kilomita zaidi ya 10 hadi kilomita 3.

Waziri wa maji katika kaunti ya kilifi Mwachitu Kiringi amesema mradi huo ni muhimu hasa wakati huu wa ukame kwa maana mabwawa na mito ya msimu imekauka.

Amesema mradi huo ulitoa maji kwenye mto Sabaki ambao uko umbali wa zaidi ya kilomita tano.

BY NEWS DESk