HabariNewsSiasa

Kinara wa ODM Raila Odinga kuzuru Pwani wikendi hii….

Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga anatarajiwa kuzuru eneo la Pwani wikendi hii kuendeleza kampeni yake ya azimio la umoja.

Kwa mujibu wa mbunge wa Mvita Abdulswamad Nassir tayari viongozi wa eneo hilo wamejiandaa kumkaribisha na kuendeleza mazungumzo kuhusu matatizo ya pwani na jinsi ya kuyatatua.

Hata hivyo haijulikani iwapo magavana wote watahudhuria ikizingatiwa kwamba baadhi ya magavana hao kama vile wa Kilifi Amason Kingi amechukua mkondo tofauti, huku wa Kwale Salim Mvurya akiwa katika chama cha jubilee, pia kuna viongozi kadhaa ambao wamejihusisha na chama cha UDA.

Hata hivyo kibarua kigumu kitakuwa kwa gavana Hassan Joho kudhihirisha kwamba bado anaweza kutegemewa na chama hicho.

BY NEWS DESK