HabariNews

WIZARA YA ELIMU YAONYA VYUO VIKUU VITAKAVYOONGEZA KARO KWAMBA VITACHUKULIWA HATUA KALI ZA KISHERIA ……….

Katibu wa elimu katika vyuo vikuu na utafiti Simon Nabukwesi amesema kuwa hakuna chuo kikuu ambacho kimeruhusiwa kuongeza karo ya shule hivyo watakaofanya hivyo watachukuliwa hatua ya kisheria.

Akizungumza katika kongamano lilowaleta pamoja wasimamizi wa chuo kikuu cha Moi katika hoteli moja hapa mommbasa katibu huyo amesema kuwa karo ya vyuo vikuu ni shilingi 16000 ambayo ni sawa kwa wazazi kuweza kulipa .

Hata hivyo amesema kuwa vyuo vikuu viwe na subra kwani tayari wizara ya elimu imetenga shilingi bilioni 2 kwa mijali ya kulipa wafanyakazi katika vyuo vikuu kote nchini.

 

BY NEWS DESK