HabariNews

Onyo kali imetolewa kwa wakazi wa Mitsemerini eneo bunge la Ganze……………..

Onyo kali imetolewa kwa wakazi wa Mitsemerini eneo bunge la Ganze kukoma kuchukua sheria mikononi kufuatia kuuawa kwa mzee wa takriban miaka 90 eneo hilo.

Akizungumza wakati wa mazishi ya mzee Mdzomba Jefwa Yaa aliyeuawa juma lililopita kwa kukatwa panga, naibu chifu wa eneo hilo Suleiman Kenga Mangi amekashifu vikali mauaji hayo akisistiza kuwa kila mtu katika taifa la Kenya ana haki ya kuishi.

Amesema tayari maafisa wa upelelezi wa jinai DCI wameanzisha uchunguzi kubaini chanzo cha mauaji ya mzee huyo huku akisema kuwa sheria itamkabili yeyote aliyehusika na mauaji hayo.

Kenga amewataka wakazi wa eneo hilo kufuatilia mafunzo ya dini, huku akieleza kuwa visa vya mauaji vinaharibu sifa za eneo hilo.

Ikumbukwe kaunti ya Kilifi ni miongoni mwa kaunti zinazoorodhesha visa vingi vya mauaji ya wazee kwa tuhuma za uchawi.

BY ERICKSON KADZEHA