HabariNewsSiasa

Seneta wa kaunti ya Baringo Gideon Moi leo anatarajiwa kukutana na viongozi na wajumbe wa chama cha KANU mjini Mombasa.

Kinara wa chama cha KANU ambaye pia ni seneta wa kaunti ya Baringo Gideon Moi leo anatarajiwa kukutana na viongozi na wajumbe wa chama hicho mjini Mombasa.

Moi kwa sasa yuko kwenye ziara ya siku tatu katika ukanda wa pwani akijaribu kuwashawishi wapiga kura wa ukanda huu kumuunga mkono katika azma yake ya kuwania kiti cha urais mwaka ujao.

Awali hio jana akizungumza huko Kwale wakati wa mkutano na viongozi na wafuasi wa chama hicho amesema kuwa mikutano itafanyika kote nchini ili kupanga mikakati inayolenga  uchaguzi wa mwaka ujao huku akidokeza kuwa muungano wa OKA bado uko imara.

Mwenyekiti huyo alikuwa ameandamana na viongozi mbali mbali wa KANU akiwemo mwakilishi wa wanawake wa Lamu Ruweida Obo, AbdiKarim Osman mbunge wa Fafi Garrissa, Manza Beja mwakilishi wadi ya Mwereni.

Baada ya ziara ya eneo hili uongozi wa KANU unatrajiwa kufanya kabla ya mkutano mkuu jijini Nairobi tarehe 30 mwezi huu kutoa maamuzi ya kumuidhinisha Moi kuwania kiti cha urais mwaka ujao.\

BY NEWS DESK