HabariLifestyleTravel

MAKUNDI YA KINA MAMA WANOJIHUSISHA NA BIDHAA ZA KITALII KAUNTI YA KWALE WAITAKA SERIKALI KUWATAFUTIA SOKO………….

Makundi ya kinamama wanaojihusisha na sanaa za usukaji wa bidhaa asilia za kitalii (vikapu ,vipepeo na mikeka na mambo ya nyumba) katika eneo la Madibwani huko Matuga kaunti ya Kwale wanaitaka serikali ya kaunti kwa ushirikiano na ile ya kitaifa kuwatafutia soko la jumla la bidhaa zao ili ziwafaidi.

Wakiongozwa na Mwanahamisi khamis Mwamulalo wanaeleza kwamba biashara hio kwa sasa haina faida kwani wanalazimika kuuza bidhaa zao kwa madalali wanaozinunua kwa bei duni mno kufuatia ukosefu wa soko hatua inayowaacha katika maisha ya umaskini.

Ni hatua wanayoitaja kuwaacha nyuma kimaendeleo.

Mgombea wa kiti cha ubunge eneo la Matuga Mwanaisha Chidzuga aliyekuwa akizungumza alipokutana na wawakilishi wa makundi ya akinamama 50 huko Madibwani ameahidi kushirikiana na makundi ya akinamama hao ili kuona kwamba wanapata soko la bidhaa zao.