AfyaHabariNews

Waziri wa afya Mutahi Kagwe amesisitiza wananchi kujitokeza na kupokea chanjo ya kuthibiti msambao wa virusi vya covid-19…

Waziri wa afya Mutahi Kagwe amesisitiza wananchi kujitokeza na kupokea chanjo ya kuthibiti msambao wa virusi vya covid-19 humu nchini ili kupata kinga thabiti dhidi ya corona.

Akizungumza katika kaunti ya Murang`a, Kagwe amesema kwamba serikali inalenga kuchanja watu wapatao milioni 5.8 ifikapo siku ya sherehe za mashujaa.

Wakati huo huo, Kagwe amesisitiza haja ya kuanzishwa kampeni za maafisa wa afya kuanza kuwachanja haswa wazee katika makaazi yao kuanzia juma lijalo.

Haya yanajiri huku taifa likirekodi visa vipya 54 vya Covid-19 baada ya sampuli 2,501 kufanyiwa vipimo chini ya saa 24 zilizopita na kujumlisha idadi ya maambukizi hadi na kufikisha idadi 248,515.

Vile vile, idadi ya Vifo nchini imeongezeka na kufikia 5,109 baada ya wagonjwa wengine 7 kuaga dunia kutokana na ugonjwa huo.

Kwa sasa, kuna wagonjwa 1,126 ambao wamelazwa katika hospitali mbalimbali nchini,  2,586 wakiwa kwenye mpango wa utunzaji na huduma ya nyumbani.

Wakati huo huo, wagonjwa 437 wamethibitishwa kupona ugonjwa huo kati yao 314 wanatoka katika mpango wa huduma za nyumbani na 123 waliruhusiwa kutoka vituo mbalimbali vya afya nchini na kujumlisha idadi ya waliopona kufikia 240,672.

BY NICKY WAITA