HabariNews

Watu wawili muendesha boda boda na abiria wake wafariki papo hapo…

Watu wawili muendesha boda boda na abiria wake wamefariki papo hapo katika eneo la Marivhenyi, bara bara ya Voi – Mwatate Kaunti ya Taita Taveta usiku wa kuamkia leo.

Inaarifiwa kwamba wawili hao waligongana ana kwa ana na lori la kubeba mizigo na kusababisha vifo vyao huku piki piki ikibondeka vibaya.

Miili ya wawili hao inahifadhiwa katika makafani ya Hospitali ya Moi Mjini Voi huku wito ukitolewa kwa wahudumu wa boda boda kuwa makini na waangalifu wanapokuwa barabarani.

Itakumbukwa kwamba ajali hiyo inafikisha watu watano waliofariki kwenye ajali zinazohusisha boda boda kaunti hiyo katika kipindi cha miezi miwili.

BY NEWS DESK