HabariNews

MSHUKIWA WA MAUAJI YA AGNES TIROP AFIKISHWA MAHAKAMANI.

Mshukiwa wa mauaji ya mwanariadha Agnes Tirop amefikishwa katika Mahakama ya Eten hii leo.

Ibrahim Rotich amefikishwa mbele ya Hakimu Mkuu wa Mahakama hiyo Charles Ekutwaa ambapo upande wa Mashtaka uliomba mda zaidi ili kufanikisha uchunguzi.

Ombi la Muendesha Mashtaka wa Serikali Judith Ayumo la mshukiwa kuzuiliwa kwa kipindi cha siku ishirini limekubaliwa huku Hakimu huyo akiagiza mshukiwa kuzuiliwa katika kituo cha Polisi cha Eldoret.

Ameagiza afanyiwe uchunguzi wa akili katika hospitali ya Rufaa ya Moi huku kesi hio ikitarajiwa kutajwa tena tarehe 9 Mwezi ujao.

Itakumbukwa kwamba mwanariadha Agns Tirop alipatikana ameaga dunia nyumbani kwake kwenye eneo la ten Katika Kaunti ya Elgeyo Marakwet Jumatano wiki iliyopita akiwa na majeraha ya kisu.

BY NEWS DESK