AfyaHabariNews

Kenya imesajili visa 151 vipya vya maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 7,224 chini ya saa 24 zilizopita.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 252,839 huku  kiwango cha maambukizi cha asilimia 2.1%.

Vile vile watu 35 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 246,390, 25 kati yao wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 10 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Watu 3 wameaga dunia kutokana na virusi vya corona huku jumla idadi ya walioaga dunia ikifika 5,263.

Kuna wagonjwa 488 ambao wamelazwa hospitalini, 1,308 wamejitenga nyumbani.

Huku hayo yakijiri kuna wagonjwa 27 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).

BY NEWS DESK.