HabariNews

Wanasiasa kaunti ya Mombasa waonywa dhidi ya kuwatumia vibaya vijana.

Idara ya polisi kaunti ya mombasa imetoa onyo kwa viongozi wa kisiasa wanaowatumia vibaya vijana kuleta virugu miongoni mwa jamii wakati huu tunapokaribia uchaguzi mkuu mwaka ujao.

Akizungumza na meza yetu ya habari naibu inspekta wa polisi kaunti ya mombasa Joseph Ongaya amesema kuwa idara ya polisi iko macho na watatumiwa mbinu zozote zile ili kuwanasa wanasiasa hao na kuwachukulia hatua za kisheria

Ongaya aidha amewahakikishia wakaazi wa mombasa na Pwani kwa ujumla usalama huku akiwataka kuishi na amani miongoni mwao akidai kuwa idara ya usalama imejipanga vilivyo katika kuhakisha kuwa amani inadumishwa.

Kwa upande wake naibu kaunti kamishna kata ndogo ya nyali Henry Rop amesema kuwa idara ya polisi itatumia baadhi ya vijana waliojisalimisha na kujirekebisha kutoka katika vikundu vya uhalifu kuwanasa vijana  ambao bado wamo katika magenge ya uhalifu kaunti ya mombasa.

BY NEWS DESK