HabariNews

Wito umetolewa kwa wakazi kaunti ya Kilifi kukoma kuwaruhusu wafugaji wa kuhamahama kulisha mifugo kwenye mashamba yao.

Akitoa wito huo mkurugenzi wa idara inayosimamia huduma za mifugo kaunti ya Kilifi Dkt Malenga Cornel, amesema wafugaji wengi wa kuhamahama wanatoka katika kaunti za Tana river na Garissa ili kuwatafutia malisho mifugo wao hali anayosema imepelekea kupungua kwa malisho katika kaunti ya Kilifi.

Maelfu ya mifugo wamekufa kaunti ya Kilifi kutokana na kukosekana kwa malisho kufuatia kushuhudiwa kwa kiangazi kikali katika maeneo mengi ya kaunti hiyo.

Aidha ameonya kuwa hatua hiyo itasaidia kupungua kwa msambao wa magonjwa yanayosambazwa na mifugo kutoka kaunti nyingine hadi Kilifi.

Ameongeza kuwa jitihada ya kutoa chanjo kwa mifugo kutasaidia mifugo kaunti hiyo kutoambukizwa magonjwa na mifugo wanaoingia kaunti ya Kilifi.

BY NEWS DESK