AfyaHabariNews

Afisa mkuu wa afya ya umma kaunti ndogo ya Tana Delta Elvis Komora amesema ni muhimu kila mwanainchi awe na choo…

Huku siku ya vyoo duniani ikiadhimishwa hapo jana kote ulimwenguni, katika kaunti ya Tana River sherehe hizo zimeadhimishwa katika mtaa wa Jua Kali mjini Garsen.

Kauli mbiu ya mwaka huu ya siku ya vyoo ikiwa ni ”kuthamini vyoo”, wakaazi wa Tana River wameshauriwa kuendelea kutumia vyoo na kuweka mazingira safi ili kuepukana na maradhi.

Afisa mkuu wa afya ya umma kaunti ndogo ya Tana Delta Elvis Komora amesema ni muhimu kila mwanainchi awe na choo akisema kuwa asilimia 80% ya wagonjwa wanaoenda hospitali wanaugua magonjwa ambayo yanaweza kuzuiwa huku akisema kwamba kati ya hayo, asilimia 50% ni magonjwa ambayo yanasababishwa na maji chafu.

Wakati huo huo Komora, amewashauri wazazi kuhakikisha wana wao wanapata chanjo zote ili kuwakinga na maradhi kama vile Polio na HPV.

amesema ipo haja ya wasichana wenye umri wa kuanzia miaka 10 hadi 14 kupata chanjo ya HPV ili kuzuia kansa ya kifuko cha uzazi.

BY NEWS DESK