HabariNews

Baraza la mitihani nchini KNEC limetoa makataa hadi novemba 30…

Baraza la mitihani nchini KNEC limetoa makataa hadi novemba 30 kwa washika dau wa elimu kuhakikisha kwamba data ya watahiniwa wanaofanya mtihani mwaka ujao zimenakiliwa vyema.
Afisa mkuu mtendaji wa KNEC David Njegere amesema kwamba marekebisho yoyote kuhusu taarifa za watahiniwa hao yanafaa kuwasilishwa kwa baraza hilo mara moja.
Miongoni mwa taarifa hizo ni mwaka wa kuzaliwa wa watahiniwa, jinisia huku majina ya watahiniwa wa kidato cha nne yakitakiwa kuowana na yale yaliyopo kwenye cheti cha kitaifa wa darasa la nane KCPE.
Aidha wanaofanya mtihani wa kitaifa wa KCPE wanafaa kuhakikisha kwamba nambari zao za mtihani zimenakiliwa vilivyo, na kulingana na kalenda ya elimu mtihani wa KCPE utafanyika kuanzia tarehe 7 mwezi machi hadi 10 mwezi huo huku ule wa KCSE ukitarajiwa kuanza mnamo tarehe 11 Machi hadi Aprili Mosi.

BY NEWS DESK