HabariNews

Kongamano la 7 la Ugatuzi linaendelea kwa siku ya pili hii leo huku suala la Mabadiliko ya hali ya anga likitarajiwa kuendelea kujadiliwa.

Kulingana na Ratiba ya hapo awali, Ilitarajiwa kwamba Kinara wa Chama cha ODM Raila Odinga angehutubu hii leo lakini alikuwa miongoni mwa Viongozi waliozungumza hapo jana kwenye Kongamano hilo lililofunguliwa rasmi na Rais Uhuru Kenyatta.
Kongamano la mwaka huu limetajwa kusaidia kutoa muelekeo kuhusu mikakati inayowekwa kukabili athari za mabadiliko ya hali ya anga.
Katika Hotuba yake Rais Uhuru Kenyatta amesema kwamba Kenya inapanga kukusanya shilingi Trilioni 6.2 zitakazotumika katika mipango ya kupunguza hewa chafu kwa asilimia 32 katika kipindi cha miaka 10 ijayo.
Wakati uo huo Rais amesema kwamba Kenya imejitolea kufadhili asilimia 13 ya kiwango hicho cha fedha ambazo ni shilingi billion 806 huku ikitarajiwa kupata nyengine kutoka kwa wafadhili mbali mbali.

BY NEWS DESK