HabariNews

RAIS UHURU KENYATTA KUONGOZA HALFA YA KUFUZU KWA MAKURUTU WALIOJIUNGA NA POLISI WA UTAWALA AP.

Usalama umeimarishwa Jijini Nairobi wakati ambapo Rais Uhuru Kenyatta kuongoza hafla ya kufuzu kwa makurutu waliojiunga na kitengo na kitengo cha polisi wa Utawala AP.
Ili kuimarisha usalama huo hata zaidi, marafiki na majamaa wa wanaofuzu wamezuiwa kuhudhuria hafla hiyo inayoendelea katika Chuo cha mafunzo ya Polisi cha Embakasi.
Wageni wachache walioalikwa wamepekuliwa mara kadhaa kabla ya kuruhusiwa kuingia katika Chuo hicho huku wakuu wa Idara ya Usalama wakisema kwamba ni mikakati ambayo imechukuliwa ili kukabili shambulio lolote la kigaidi.