HabariNews

Baraza la wazee wa jamii ya waluo eneo bunge la Nyali kaunti ya Mombasa wameeleza azima yao ya kumuunga mkono kiongozi mwenye msimamo na uaminifu kwa chama cha ODM.

Baraza la wazee wa jamii ya waluo eneo bunge la Nyali kaunti ya Mombasa wameeleza azima yao ya kumuunga mkono kiongozi mwenye msimamo na uaminifu kwa chama cha ODM.
Akizungumza katika Wadi ya frere Town eneo bunge la Nyali katika kikao cha kujadili miradi mbali mbali itakayoinua jamii hiyo kimaendeleo, baraza hilo likiongozwa na mwenyekiti wake Obara James Kings limeshikilia msimamo wake wa kumuunga mkono kiongozi ambaye ana msimamo na uaminifu kwa chama cha ODM na kinara wa chama hicho Raila Odinga.
Huku uteuzi wa vyama ukikaribia, baraza hilo limesema liko tayari kumuunga mkono na kumuidhinisha mbunge wa mvita Abdulswamad Shariff Nassir kuwania kiti cha ugavana kaunti ya Mombasa kutokana na uaminifu na msimamo wake kwa chama cha ODM.
Haya yanajiri huku Nassir akiendeleza kampeni zake za kumpigia debe kinara wa Chama cha ODM Raila Odinga kuwa rais wa tano wa jamhuri ya taifa la Kenya.
Nassir amemtaja Odinga kama mkombozi na ambaye ataweza kulikomboa taifa la Kenya huku akikemea vikali siasa zenye kuleta mgawanyiko,chuki na ukabila .

BY NEWSDESK