HabariNews

wazazi kaunti ya Mombasa waunga mkono pendekezo la Profesa George Magoha la kurudisha adhabu ya kiboko shuleni.

Huku visa vya kukosa nidhamu shuleni vikizidi kushuhudiwa katika shule mbalimbali hapa nchini wazazi pamoja na walimu wanapendekeza kurejeshwa kwa adhabu ya kiboko shuleni.
Kulingana na wazazi hao ni kwamba watoto wanakosa adabu kutokana na kutoadhibiwa hali ambayo wanasema imewachangia wao kutowaheshimu wazazi pamoja na walimu shuleni,huku wakiongeza kwamba mzazi yeyote atakaye mtetea mwanawe kwa kuadhibiwa pia achukuliwe hatua.
Aidha kulinga na Mwalimu Erick ambaye ni mwalimu katika shule moja ya msingi hapa jijini mombasa,wazazi wanapaswa kuwafundisha maadili mema na kuongeza kwamba wazazi wanapaswa kutowatetea wanao wanapoitwa shuleni kuhusiana na makosa ambayo wamefanya.
Haya yanajiri baada ya waziri wa elimu George Magoha pamoja na yule wa usalama wa ndani Fred Matiang’I kupendekeza kurejeshwa adhabu ya kiboko shuleni ili nidhamu irudi miongoni mwa watoto.

BY NEWSDESK