HabariNewsSiasa

Gavana wa Kaunti ya Kilifi Amason Kingi sasa anasema anaunga mkono azma ya Kinara wa Chama cha ODM Raila Odinga kuwania Urais mwaka ujao.

Ni takriban Miezi mitano tu baada ya kujiondoa katika Chama cha ODM kufutia hatua ya kupokonywa uwenye kiti wa Chama katika Kaunti ya Kilifi, Gavana wa Kaunti hiyo Amason Kingi sasa anasema anaunga mkono azma ya Kinara wa Chama cha ODM Raila Odinga kuwania Urais mwaka ujao.
Kingi ambaye hapo awali amekuwa akikosoa uongozi wa ODM na hata kutarajiwa kujiunga na mrengo wa Naibu wa Rais William Ruto au Muungano wa One Kenya Alliance (OKA), amesema kwamba atamfanyia kampeni Odinga ili kupiga jeki uungwaji mkono wa Raila katika eneo la Pwani na hasa katika Kaunti ya Kilifi.
Wakati uo huo Kingi, ambaye alianzisha Chama chake cha Pamoja African Alliance (PAA) ili kuwajumuisha wanasiasa wa Pwani, amesema kwamba Chama hicho kitakuwa na mgombea wa Urais, japo kutakuwa na wagombea wengine katika yadhifa nyengine.
Itakumbukwa kwamba Gavana Kingi alifurushwa katika Chama cha ODM miezi mitano iliyopita baada ya kushikilia msimamo wa kuanzisha Chama tofauti katika eneo la Pwani kinyume na msimamo wa Chama cha ODM.

BY NEWSDESK