HabariNews

Wahudumu wa magari ya usafiri wa umma wailaumu serikali.

Wahudumu wa magari ya usafiri wa umma wanailaumu serikali kuwa imechangia pakubwa katika kudorora kwa kazi yao wakti huu wa sherehe za krismasi pamoja na mwaka mpya
Kulingana na wahudumu hao usafiri wa SGR umechangia pakubwa katika kudorora kwa kazi yao kwani wasafiri wengi wanatumia sana usafiri huo hivyo basi kuchangia katika ukosefu wa abiria ambao ni tegemeo kubwa kwao.
Aidha wamesema kuwa uksefu wa ajira umewafanya kupunguza nauli jambo ambalo limeathiri mapato yao
Baadhi ya wasafiri aidha wamesema kuwa idadi ndogo nya wasafiri inayoshuhudiwa inawaathiri pia nao kwani inawalazimu kukaa katika kituo cha mabasi muda mrefu wakisubiria gari kujaa.

BY NEWSDESK