HabariNews

MITIHANI YA KITAIFA YA K.C.P.E NA K.C.S.E KUFANYIKA JINSI ILIVYOPANGWA ASEMA WAZIRI GEORGE MAGOHA.

Shughuli za masomo zinarejelewa hii leo kote Nchini kwa muhula wa tatu wa mwaka 2021.
Kulingana na Kalenda ya masomo ni kwamba shule zote zitafunguliwa hii leo wiki moja tu baada ya kufungwa kwa likizo za Krisimasi na mwaka Mpya.
Ikumbukwa kwamba Waziri wa Elimu Profesa George Magoha, alikataa pendekezo la waalimu waliotaka tarehe ya mitihani kusongeshwa mbele ili kuwapa fursa ya kumaliza selabasi akisema kwamba mitihani hiyo itafanyika jinsi ilivyopangwa.
Muhula wa 3 wa mwaka wa masomo wa mwaka 2022 utakuwa wa wiki tisa kabla ya kupisha mitihani ya Kitaifa ya darasa la nane KCPE na kidato cha nne KCSE.
Mitihani ya KCSE itafanyika kwa siku nne kuanzia tarehe 7 hadi 10 mwezi wa tatu huku ile ya KCSE ikitarajiwa kuchukua wiki tatu, kuanzia tarehe 11 Machi hadi Mosi Mwezi Aprili. Shughuli ya usahihishaji pia ikitarajiwa kuchukua wiki tatu kuanzia Aprili nne hadi Aprili 22.
Aidha mwaka uu huu wa 2022, utakuwa wa mihula minne ya masomo huku mitihani mengine ya Kitaifa ikiwa imeratibiwa mwezi Novemba japo tarehe kamili haijatolewa.
Itakumbukwa kwamba Kalenda ya masomo iliathirika baada ya shule kufungwa kwa takriban miezi 9 mwaka jana na itarejelewa kawaida kuanzia mwaka 2023 ambapo muhula wa kwanza utaanza rasmi mwezi Januari tarehe 23.

BY NEWSDESK