HabariLifestyleNews

Afisa wa polisi amejiua kwa kujipiga risasi, Mombasa.

Afisa wa polisi amejiua kwa kujipiga risasi na bunduki yake ya kazi aina ya G3 katika makaazi ya polisi eneo la Makupa, Kaunti ya Mombasa usiku wa kuamkia leo.
Kulingana na maafisa wenzake walioshuhudia tukio hilo ni kwamba Konstabo Jacob Masha mwenye umri wa miaka 32, ametumia bunduki yake kujipiga risasi ndani ya nyumba yake.
Kamanda wa polisi wa eneo hilo Manasseh Musyoka amesema kwamba wanachunguza tukio hilo ili kubaini chanzo cha tukio hilo.
Mwili wa marehemu unahidhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya rufaa ya Coast General. 
Hili ni tukio la hivi punde la afisa wa polisi kujitoa uhai katika msururu unaohusishwa na masuala ya kisaikolojia na itakumbukwa kwamba Kitengo cha ushauri nasaha kilianzishwa ndani ya huduma za polisi ili kuwasaidia maafisa hao kujikwamua kutoka kwa msongo wa mawazo.