HabariNewsWorld

Rais wa Taifa la Hungary Yánosh Áder yuko humu Nchini kwa ziara ya siku nne.

Rais wa Taifa la Hungary Yánosh Áder yuko humu Nchini kwa ziara ya siku nne. Rais huyo ambaye ameandamana na mkewe Anita Herczech amepokelewa katika Uwanja wa Kimataifa wa ndege ya Jommo Kenyatta na Waziri wa masuala ya Kigeni Racheal Omamo. Rais Uhuru Kenyatta amempokea mgeni wake katika ikulu ya rais jijini Nairobi. Rais Ader amepigiwa mizinga ishirini na moja na wanajeshi wa majini na kisha kulikagua gwaride. Rais huyo anatarajiwa kushiriki mazungumzo ya kuboresha uhusiano wa kidiplomasia na kibiashara na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta. Ikumbukwe kwamba Taifa la Hungary limekuwa na uhusiano wa kidiplomasia na Kenya tangu mwaka 1964.