HabariNewsSiasa

USAJILI WA WAPIGA KURA KWA AWAMU YA PILI YAANZA HII LEO.

Huku usajili wa wapiga kura ukianza rasmi hii leo, wito umetolewa kwa wananchi ambao bado hawajasajiliwa kujitokeza kwa wingi haraka iwezekanavyo.
Wakizungumza katika eneo bunge la Likoni Kaunti ya Mombasa, Mbunge wa eneo hilo Mishi Mboko na mwenzake wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir, wamesema kwamba kuna umuhimu kwa wale ambao hawajajisajili kujitokeza kwa wingi ili kuwachagua viongozi walio bora.