HabariNews

Maafisa kumi wakuu wa Kenya Power wanatarajiwa kufikishwa Mahakamani.

Maafisa kumi wakuu wa Kenya Power wanatarajiwa kufikishwa Mahakamani baada ya kukamatwa hapo jana kwa kosa la kutatiza usambazaji wa umeme ambao umeathiri kaunti zaidi ya kumi na tano wiki iliyopita.
Kumi hao wakiwemo meneja mkuu wa usambaji wa umeme wameshtakiwa na mashtaka ya utepetevu baada ya kutakiwa kujisalimisha katika makao makuu ya idara ya upelelezi DCI na kisha kusafirishwa hadi kituo cha polisi cha Muthaiga. Itakumbukwa kwamba Juma lililopita, mkuu wa DCI George Kinoti aliagiza kukamatwa na kuhojiwa kwa maafisa hao baada ya kubainika kwamba jopo kazi la Kenya power lilikuwa limewasilisha ripoti kwa bodi ya kampuni hiyo tarehe nane mwezi Disemba likipendeza kukarabatiwa kwa nyaya za umeme eneo la Embakasi.