HabariNews

Muungano wa Makanisa kutoka Mpeketoni kaunti ta Lamu unataka serikali kuajiri maafisa wa polisi wa akiba ili kuimarisha usalama eneo la Mpeketoni na viunga vyake.

Muungano wa Makanisa kutoka Mpeketoni kaunti ta Lamu unataka serikali kuajiri maafisa wa polisi wa akiba ili kuimarisha usalama eneo la Mpeketoni na viunga vyake.

Maaskofu wa muungano huo wakiongozwa na Askofu Noel Kitese, aidha wameonya vijana na viongozi wa siasa dhidi ya kutumia maneno ya uchochezi kwenye mikutano ya hadhara ama hata mitandaoni.
Waumini hao wameyasema haya wakati wa ziara ya kugawanya chakula na mavazi kwa familia zilizoathirika na mashambulizi yaliyotekelezwa katika maeneo ya Widho, Salama na Juhudi katika wadi ya Hindi ambapo watu kadhaa waliuawa.
Hata hivyo baadhi ya waathiriwa wakiwemo watoto wachanga na akina mama wajawazito ambao wanalala nje, wanaitaka serikali kuimarisha usalama ili waweze kurudi maeneo yao.