FoodHabariNews

Zaidi ya wakulima elfu 13 kutoka kaunti za Kwale, Kilifi, Taita Taveta wamepokea fidia ya milioni 84 kutoka kwa bima ya wizara ya kilimo nchini.

Zaidi ya wakulima elfu 13 kutoka kaunti za Kwale, Kilifi, Taita Taveta wamepokea fidia ya milioni 84 kutoka kwa bima ya wizara ya kilimo nchini.
Kulingana na wizara ya kilimo fidia hiyo itakwenda kwa wakulima waliokuwa na bima na kupoteza mazao yao kufuatia ukame.
Akizungumza na waandishi wa habarikatibu wakilifo nchini Prof Hamadi Boga,amewahimiza wakulima kujisaljili kwenye bima ya kilimo ili kujiepusha na mabadiliko na hali yaanga.
Ni kauli iliyoungwa mkono na waziri wa kilimo katika serikali ya kaunti ya Kwale Joan Nyamasyo ,akiwahimiza wakulima kuchukua bima hizo ili kuhakikisha kwamba wanalinda mimea yao hata wanapokosa mavuno.
Kati ya kaunti zilizoorodheshwa kupokea bima hizo ni pamoja na Kaunti ya Kwale Kilifi na Taita taveta mtawalia ambapo wakulima kaunti ya Kwale wamepata milioni 13.9, Kilifi Milioni 56, huku Taita ikipata milioni 14.