HabariNews

Serikali ya kaunti ya Kilifi yalaumiwa.

Serikali ya kaunti ya Kilifi imelaumiwa kwa kosa kuwa na mbinu mbadala ya kuja na bodi ya kusimamia usambazaji wa maji kaunti hiyo.
Kulingana na spika wa bunge wa kaunti hiyo Jimmy kahindi, ukosefu wa uadilifu na uongozi mbaya umetajwa kuwa donda sugu kwa kaunti hiyo kutokana na ufujaji wa mali ya umma ambao imepelekea kaunti hiyo kuwa na ardhi kame kwa ukosefu wa maji.
Kahindi amesema kuwa serikali ya kaunti ya Kilifi iko na rasilimali ya kutosha kufanya miradi tofauti moja wapo ikiwa ya kuchimba visa maeneo tofauti ambavyo vitasaidia pakubwa kumaliza tatizo la ukosefu maji katika kaunti hiyo.

BY EDITORIAL DESK