HabariNews

Gavana wa kaunti ya lamu ashindwa kuwasidia wakaazi wa kaunti hiyo.,

Mwanaharakati wa kijamii kaunti ya Lamu Yunus Ishaq amemkosoa gavana wa kaunti hiyo Fahim Yasin Twaha kwa kile alichokitaja kuwa amekosa kusaidia jamii wavuvi wa Lamu licha ya kuwa mwenyekiti wa uchumi samawati almaarufu kama Blue Economy .
Kulingana na Ishaq ,sekta ya uvuvi na uchumi samawati ni miongoni mwa vitega uchumi vikuu vinavyotegemewa na wakaazi wengi kaunti ya Lamu lakini sector hizo gavana amekosa kuziimarisha kwa kujenga kiwanda cha uvuvi.
Aidha ameongeza kuwa haoni umuhimu wowote wa gavaa Twaha kuchaguliwa kama mwenyekiti wa blue Economy kwa awamu ya pili mfululizo kutokana na kudorora kwa sekta hizo muhimu Lamu.

BY EDITORIAL DESK