Rais Uhuru Kenyatta ametia sahii miswada 5 kuwa sheria moja wapo mswada wa bajeti ya ziada ambayo ulipitishwa mapema wiki iliyopita.
Wakati huo huo Rais Kenyatta ametoa shilingi bilioni 34.44 kutoka bajeti ya ziada katika idara husika na biashara ya mafuta nchini ili kuwanusuru wakenya ambao wamekuwa katika hali tete ya uhaba wa mafuta nchini.
Haya yanajiri saa chache baada ya wafanyibiashara katika sekta ya uchukuzi pamoja wakenya wakawaida wanaotumia bidha ya mafuta kulilia uhaba wa mafuta nchini baada ya bidha hiyo kukosekana kwa muda wa wiki moja kufikia sasa.
Hata hiyo bajeti hiyo za ziada ya fedha imejumuisha Zaidi ya shilingi bilioni 139.75 ambayo itatumika katika kukabiliana na baa la njaa, maandalizi ya uchaguzi ,kuboresha usalama wa taifa, kuboresha bei ya mafuta miongoni mwa majukumu mengine.