BurudaniEntertainmentHabariNews

LUWI CAPELLO APATA UA KUTOKA KWAO NYUMBANI, POKOMO PRINCESS.

Rachel Maliwa almaarufu kama Pokomo Princess ambaye ni mwanamziki mashuhuri kutoka Tanariver Kaunti 004, ni wa hivi karibuni kuonekana katika picha zilizofikia meza yetu ya babari wakiwa pamoja na mwigizaji almaarufu Luwi Capello.

Tetesi ni kwamba wawili hao wamekuwa katika mahusiano ya kimapenzi yalioanza takriban miezi mitatu iliyopita na vilevile kutokana na picha za kimahaba zilizovuja mitandaoni ambazo zimezua gumzo kutoka mashabiki wao.

Banjamin Komora almaarufu kama Luwi Capello ambaye amekuwa katika Nairobi diaries na vipindi kama vile Aziza, aliachana na mchumba wake wa zamani, Pendo mwaka wa 2017 kwa tetesi kuwa alimwendea kinyume Luwi.

Kwa upande wake Pendo, alikiri madai hayo na kwamba alifurahia.

Ikiwa wawili hao wako katika mahusiano ya kimapenzi huenda wakawa “power couple” kutokana na kauli kwamba wote ni Wapokomo.

Ama kweli Mwenda tezi na omo marejeo ngamani, Luwi alizunguka kote lakini akapata mapenzi ya dhati kutoka kwao nyumbani, mpenzi akiwa Pokomo Princess.

Kwa sasa unaweza burudika na EP ya “TSEA” yake Pokomo Princess aliyoidondosha hivi majuzi.

BY LEON NKADUDA