HabariNews

Wakaazi wa Kinango walalamikia uhaba wa maji.

Wakaazi wa Kinango kaunti ya Kwale sasa wanahofia kukumbwa na mkurupuko wa magonjwa kutokana na tatizo la uhaba wa maji katika eneo hilo.

Wakaazi hao wakiongozwa na Francis Maluki, wamesema kuwa tatizo hilo linatishia pakubwa afya zao kufuatia ukosefu wa maji katika sehemu za umma.

Wamedai kuwa baadhi ya sehemu hizo kama vile hospitali, vichinjio na maeneo ya kuuza chakula yamekosa maji safi ya matumizi kwa binadamu.

Kwa upande wake naibu gavana wa Kwale Chirema Kombo amekanusha madai hayo baada ya wakaazi hao kuandamana kulalamikia uhaba wa maji katika eneo hilo kwa muda mrefu.

Kombo amedokeza kuwa tayari kampuni ya kusambaza maji Kwale (KWAWASCO) imelishughulikia tatizo hilo ambalo limekuwepo kwa muda wa siku mbili tu kutokana na ukosefu wa nguvu za umeme.

BY EDITORIAL DESK