Uncategorized

Zaidi ya vijana 600 Mombasa kusaidiwa kupata mafunzo na ajira kutoka kwa mashirika ya kijamii.

Taasisi ya Vyombo vya Habari vya Kidigitali barani Afrika ya The Afrika Digital Media (ADMI) na shirika la vijana la Global Opportunity Youth Network, wamtia saini ya makubaliano ya kusaidia vijana 600 walioacha shule na wasio na ajira katika kaunti ya Mombasa.

Mashirika hayo yamewafungulia vijana hao mradi wa mabilioni ya dola wa kampuni ya filamu.

Ushirikiano huo wa kimkakati, utatoa ya mafunzo kwa vijana na kuwaunganisha na nafasi za kazi kupitia wakfu wa Swahilipot unaokuza talanta za vijana mjini Mombasa.

Akiongea wakati kutia saini makubaliano hayo ya ushirikia mjini MOMBASA, Mkurugenzi mkuu wa taasisi ya ADMI Dr.Laila Macharia ,amesema ushikiriano huo utasaidia kutengeza ajira kwa vijana kati ya umri wa miaka 15-29 zinazotokana na ubunifu.

Kwa upande wake Daisy Chesang, afisaa mkuu wa uchumi wa ubunifu katika shirika la Global Opportunity Youth Network, anasema kuwa mafunmzo hayo yatawachonga vijana katika ajira za rasmi na zisizo rasmi katika sekta zote za ajira.

Aidha mkurugenzi mtendai wa Swahilipot Mahmoud Noor, anasema kuwa ulimwengu wa ajira umebadilika na kwa sasa nafasi nyingi za ajira zinatokana na elimu ya kiteknolojia.

Ushirikiano huo utatoa mafunzo ya kodi mbalimbali za masomo ,ikiwemo uzalishaji wa filamu na televisheni, Uzalishaji wa Video, Uwanahabari wa kidijitali, uzalishajji wa mziki pamoja na usanifu wa picha.