HabariNews

Kilio cha Haki Msichana wa miaka 12 Akiuwawa na kutupwa Kichakani, Nakuru

Familia moja eneo la Kasambara kata ndogo ya Giligil, Nakuru inaliia haki kutokana na mauajji ya mwana wao mwenye umri wa miaka 12.

Jasmine Njoki mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya Nakuru Roots Academy alinyan’anywa maisha yake angali mchanga na wauwaji wasiotambulika Jumanne usiku alipokua njiani akiregea kutoka shuleni na kisha mwili wake kutupwa kichakani.

Afisa mkuu wa upelelezi alifichua kwa taifa kua chembe chembe za ushahizi zilichukuliwa na zitapelekwa katika maambara ya kitaifa jijini Nairobi kwa ukakuzi zaidi ili kusaidi kuwaska wauwaji.

Tunaendelea kukusana pamoja ushahitdi utkaotuwezesha kuwanasa wauwaji wa Jasmin” alisema

Uchunguzi wa awali uliofanya na maafisa kutoka kitengo cha upelelezi wa makosa ya jinai DCI ulibaini kuwa kuwa mtoto huyo alinajisiwa kabla ya kuuwawa kinyama.

Kulingana na msemaji wa familia hio James Mutungi , mwili wa mwana wao ulipatikana pembizoni mwa barabra ya reli mita 800 kutoka nyumbani kwao, familia hio walipiga ripoti polisi ambao walikuja nakuuchukua mwili wa marehemu na kuupeleka katika chumba cha uhifatdhi wa maiti Gilgil ukisubiria upasuaji.

Alishukishwa na basi la shule sehemu anaposhukia kila siku. Jasmin alipotea akiwa njiani kuja nyumbani. Tukio hilo limewaacha wanafamilia na mshuko na wamepoteza tamaa” Alisema Mutungi.

Kamana wapolisi katika kata ndogo ya Gilgil Francis Tumbo hata hivyo alisema kuwa maafisa wa polisi wameanzisha uchunguzi zaidi huku maafisa ziada wakiongezwa kushika doria katika eneo hilo.

BY EDITORIAL DESK