HabariNews

Shughuli ya kutambua Miili 429 Shakahola huenda ikachukua miezi 6

Huenda mchakato wa kisayansi wa kutambua miili 429 iliyofukuliwa msitu wa Shakahola kaunti ya Kilifi ukachukua angalau muda wa miezi sita.

Kwa mujibu wa wataalamu wa vipimo vya maabara wa idara ya upelelezi DCI mchakato wa uchukuajia wa sampuli za DNA umechukua mda mrefu kufuatia kiwango cha kuharibika kwa miili hiyo.

Kati ya miili 429 iliyofukuliwa miili 360 ilikuwa imeharibika kupita kiasi, miili 48 ikiharibika kwa wastani huku miili 12 ikiharibika kidogo na miili 7 ilikuwa haijaharibika.

Idara ya DCI ilisema kuwa huenda baadhi ya matokeo ya DNA ikakosa kuwa sahihi kutokana na kiwango cha juu cha kuharibika kwa baadhi ya miili hiyo.

Kadhalika DCI ilishauriwa kuchukua muda wa kati ya siku 2 na 14 kuchunguza kila sampuli ya miili.

Haya yanajiri huku awapu ya 5 ya ufukuaji wa miili kwenye msitu huo ikitarajiwa kuendelea wiki kadhaa zijazo.

BY EDITORIAL DESK