HabariNews

KEBS Yawataka Wauzaji na Wanunuzi kuwa Makini na wanapofanya Manunuzi

Wauzaji na wanunuzi wa bidhaa mbalimbali wamehimizwa kuwa makini kuuziwa bidhaa gushi zisizo na nembo ya shirika la kutathimini ubora wa bidhaa humu nchini (KEBS).

Kulingana na mwakilishi wa shirika hilo ukanda wa Pwani Hilda Keror  wauzaji wengi wanauza bidhaa bila kuwa na nembo maalum ya shirika hilo huku akiwaonya wale wote wanaofanya biashaza hizo kuwa makini.

Hilda aliweza kutoa nambari maalum itakayotumika na kusaidia wafanyabiasha kwa kutumia simu zao kufanya uchunguzi wa bidhaa hizo kama ni sahihi au gushi kwa kuscani nambari za siri au kutuma ujumbe kwa nambari maalum kwa shirika hilo ambayo ni 22023.

Tumekuja hapa ili kutoa hamasa kwa vijana,wamama na wahudumu pamoja na wanahabari ili kupata ufahamu kuhusiana na bidhaa tunazotoa kwa umma,huku lengo kuu nikuwawezesha kutambua kati ya bidhaa gushi na halisia kwa kutumia simu zao ku-scan code iliyoko kwa bidhaa husika ili kujua uhalisia wa bidhaa hiyo au wafanyabiashara watutumie ujumbe mfupi kwa nambari 22023 ili kujua uhalisia wa bidhaa hizo”.Alisema Hilda.

Wakati huo huo Keror alidokeza uwepo wa wafanyakazi nyanjani wanaochunguza bidhaa mbalimbali ili kuhakikisha ubora wa bidhaa hizo huku akiwahimiza wasambazaji bidhaa kuchunguza bidhaa zao ili kuhakikishia uhalisia wa bidhaa hizo.

Tuko na wahudumu wetu nyanjani wanaochunguza bidhaa malimbali na tunawaomba wafanyabiashra wetu wawe makini wasihadaiwe na watu wanaouza bidhaa zisizo halali”.Alisisitiza Hilda.

BY JAPHET MAKANAKI