HabariNews

Ushirikina wachangia mimba za utotoni Kilifi

Ushirikina ni baadhi ya mambo ambayo yametajwa kuchangia ongezeko la mimba za utotoni kaunti ya Kilifi.

Wazazi wakitaka kutafutwa kwa mbinu hizo za kishirikina kusitishwa ili kufanikisha kampeni ya kuwanusuru wasichana wadogo kutonaswa kwenye mtego huo.

Kulingana na utafiti ambao ulifanywa na mhadhiri wa chuo kikuu cha pwani katika kitengo cha utabibu Doris Nguzo, wazazi walieleza kuwa vijana wamegeukia mbinu za kishirikina maarufu wende kwa lugha ya mama, ili kuwapata wasichana wanaowatamani.

Alisema mbinu hiyo imeleta changamoto ya kudhibiti hali hiyo inayozidi kutatiza jamii.

Nguzo aidha aliitaka wizara ya elimu kujumuisha kwenye mtaala wa elimu ya umilisi somo litakaloangazia madhara ya yanayotokana na mimba za utotoni.

Hata hivyo alieleza kuwa iwapo mbinu za kisayansi zitashindwa kutatua swala hilo basi jamii inafaa kutafuta mbinu za kinyumbani kukabiliana na changamoto hiyo.

By Erickson Kadzeha