Habari

Wagonjwa Kusubiri Zaidi Huduma za Afya katika Hospitali za Umma,

Wagonjwa wataendelea kutaabika na kusubiri kwa muda zaidi kupata huduma za afya katika hospitali za umma ambako madaktari wamegoma na kususia kazi wakishinikiza Serikali kutekeleza matakwa yao.

Haya ni kufuatia hatua ya Mwanasheria Mkuu nchini Justin Muturi kuitaka mahakama iwape serikali muda zaidi kuendelea kushughulikia mazungumzo kuhusu mgomo wa madaktari unaoendelea.

Mwanasheria Mkuu kupitia Wakili wake Ochieng Oduol ameiambia mahakama kuwa Serikali imepigia hatua katika mazungumzo hayo na kwamba tayari wameandikisha ripoti hitajika katika mahakama.

Akiwa mbele ya Hakimu Byram Ongara, Mwanasheria Mkuu huyo ameitaka mahakama hiyo kurefusha maagizo ya kusitisha mgomo wa madaktari chini ya chama chao cha KMPDU, sawia na kuitaka mahakama hiyo iwafungulie mashtaka viongozi wa wao kwa kudharau maagizo ya mahakama ya kuusitisha mgomo wao unaoendelea.

BY MJOMBA RASHID