HabariNews

Maafisa wa Serikali wenye Vyeti Bandia Wasamehewe Wakishajiuzulu, asema Naibu Spika Bunge la Kitaifa

Naibu Spika wa Bunge la Kitaifa Gladys Boss sasa
anapendekeza kuwa Serikali iwape msamaha maafisa
walio na vyeti ghushi wanaohudumu katika afisi za
umma.

Akizungumza katika kipindi cha mahojiano ya Asubuhi na Ruinga
moja nchini Gladys amesema maafisa hao wanastahiki
kusamehewa kwa sharti kuwa wajiuzulu.

Naibu Spika huyo wa Kitaifa anasema kuwa vita dhidi ya maafisa
wenye vyeti feki katika Huduma za umma vitakabiliwa vilivyo
iwapo serikali iaruhusu maafisa wa umma walio na vyeti bandia
kujiuzulu pasi hofu wala woga wa kufuatiliwa na kushtakiwa
baadaye.

Kauli yake inajiri huku Tume ya Huduma za Umma (PSC), Tume
ya Maadili na Kupambana na Ufisadi, EACC na Idara ya Upelelezi
wa Jinai, DCI zikiendelea kuwasaka ili kuwaondoa maafisa wa
umma walio nav yeti ghushi vya masomo.

BY NEWSDESK