HabariNews

BUNGE LA KAUNTI YA MOMBASA NA SHIRIKA LA HAKI JAMII KUSHIRIKIANA

Bunge la kaunti ya Mombasa pamoja na shirika la Haki Jamii leo wametia
saini mkataba wa makubaliano MOU wa kushirikiana katika kutekeleza
sheria na kutengeza sera za maswala ya kijamii zinazomuhusu mwananchi
katika kutatua changamoto za kijamii.

Akitia saini mkataba huo spika wa bunge la kaunti ya Mombasa Ahrub
khatri ameeleza kuwa ushirikiano huo baina ya bunge la kaunti kupitia
kamati ya afya ya bunge la kaunti ya Mombasa kutasaidia pakubwa katika
uundwaji wa sera na utekelezwaji wa sera hizi kwa kuzingatia matakwa ya
mwananchi kupata huduma bora hasa katika sekta ya afya.

Aidha naibu mkurugenzi katika shirika la Haki Jamii Lucy Baraza ameeleza
kuwa wameafikia makubaliano hayo baada ya kufanya utafiti wa baadhi ya
sheria za kaunti ya Mombasa za afya na kubaini kuwa kuna mianya mingi
katika sheria hizo ambazo zinafaa kuzibwa kwa kuja na sheria na kanuni za
kuboresha afya ya jamii ya Mombasa.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya afya ya bunge la kaunti ya
Mombasa Bernad Ogutu ameahidi kuwa kupitia kamati yake watahakikisha
kuwa mapendekezo hay yanatiliwa maanani ikiwemo kubadilisha baadhi ya
vipengee vya sheria ya afya ya kaunti hiyo na ikiwemo kumpa mwananchi
fursa ya kuchangia kutoa maoni ya jinsi ya kuimarisha huduma za afya.

Spika Ahrub amekiri kuwepo kwa mapungufu si haba katika kutoa
huduma ya afya kaunti ya Mombasa huku akieleza kuwa tatizo
ambalo linamkera mwananchi wa Mombasa ni gharama ya juu ya matibabu katika
hospitali za umma.
kama gharama za matiobabu katika hospitali za umma ni sawa na zile za
hospitali za kibinafsi hakuna haja ya kuwepo kwa hospitali za umma” Ahrub amesema.

Shirika la Haki Jamii limeeleza kuwa mbali na maswala ya afya pia
litashirikiana katika maswala ya ardhi, maji na usafi miongoni mwa
malengo yao ya kushirikiana na bunge la kaunti hiyo.
Mkataba huo wa makubaliano utatekelezwa kwa muda wa miaka minne kuanzia
siku ya kutiwa saini.
BY SOPHIA ABDHI