HabariKimataifaLifestyleTravel

Wafanyakazi 2 wa Ndege ya KQ Wakamatwa na Jeshi nchini DR Congo

Wafanyakazi wawili wa Shirika la Ndege KQ wamekamatwa mjini Kinshasa mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Katika taarifa inayothibitisha kukamatwa kwao iliyotolewa leo, Afisa Mkuu Mtendaji wa KQ, Allan Kilavuka amesema wafanyakazi hao wawili wamekamatwa na Kitengo cha Kijasusi cha Jeshi mjini Kinshasa kuhusu madai ya Kukosekana kwa hati maalum za shehena ya thamani.’

Inadaiwa kuwa sababu ya kukamtwa kwao ni kukosa hati maalum za shehena ya thamani ambayo ilikuwa isafirishwe kwa ndege ya KQ mnamo Aprili 12, 2024, hata hivyo KQ ikisema kuwa shehena husika haikusafirishwa wala kukubaliwa na KQ.

Sababu ya kukamtwa kwao ilidaiwa kuwa kukosa hati maalum za shehena ya thamani ambayo iikuwa isafirishwe kwa ndege ya KQ mnamo Aprili 12, 2024. Hata hivyo, tungependa kuaini kuwa shehena hiyo haikuchukuliwa au kukubaliwa na KQ kutokana na kutokamilika kwa nyaraka.”

Kilavuka hata hivyo amekosoa mamlaka mjini Kinshasa kwa kuwakamata wawili hao ambao ni raia wamekuwa wakizuiliwa katika kituo cha kijasusi cha kijeshi kinyume cha agizo la mahakama.

Licha ya maagizo ya mahakama, kitengo cha kijasusi cha kijeshi bado kinawashikilia kwa siri, lakini hawa ni raia wanaoshikiliwa kwa siri katika kituo cha kijasusi cha kijeshi.” Alisema Kilavuka.

Kulingana na KQ wakati wa kukamatwa kwao simu za wawili hao zilizuiliwa na hivyo kuwanyima njia zote za kuwafikia.

Mnamo Aprili 23, 2024, maofisa wa ubalozi wa Kenya na baadhi ya wafanyakazi wa KQ waliruhusiwa kuwatembelea lakini kwa dakika tu chache,” alisema Kilavuka.

Na kuhusiana na shehena hiyo, Kilavuka anashikilia kuwa haikusafirishwa kwani haikuwa katika upande wa bidhaa za kusafirishwa.

Shehena hiyo haikuwa upande wa usafiri wa angani, na kwa hivyo haikuwa mikononi mwa KQ kwa kuwa mhusika wa kusimamia mizigo alikuwa angali kukamilisha kuweka nyaraka kabla ya kuikabidhi kwa KQ. Alisema.

Bw. Kivaluka ameongeza kuwa shehena hiyo ilikuwa bado ingali kwenye sehemu ya mizigo ikifanyiwa ukaguzi wa kuidhinishwa wakati maafisa wa Usalama walifika na kudai kuwa KQ ilikuwa ikisafirisha shehena bila kibali cha forodha.

BY MJOMBA RASHID