HabariNewsUncategorized

One man, One vote, One shilling, wachana nayo!

Mbunge wa EALA Hassan Omar Sarai amemshutumu Naibu Rais Rigathi Gachagua kwa kuunga mkono pendekezo kwamba ugavi wa mapato ya serikali katika maeneo mbalimbali nchini ufanywe kwa msingi wa idadi ya watu.

Akihutubia umma katika mkutano wa hadhara wa kampeni za chaguzi za mashinani za Chama Cha UDA ulioandaliwa eneo Bunge la Nyali mjini Mombasa, mbunge huyo alisema wao kama viongozi kutoka maeneo yaliyo na idadi dogo ya watu na yaliyosalia nyuma kimaendeleo nchini watapinga vikali sera hiyo kwani itayatenga maeneo hayo kimaendeleo hata zaidi.

“Haya nayasema kwa heshima kubwa kwa Naibu wa Rais Rigathi Gachagua.Hii mambo ya one man, one vote, one shilling wachana nayo. Hiyo itatuletea uhasama mkubwa sana ndani ya hii kenya.Wajua ukitaka kuhesabu watu na one shilling, kuna baadhi ya jamii zina idadi kubwa ya watu kuliko nyingine. Taifa la Kenya linaongozwa kwa msingi wa kikatiba. Hiyo mambo ya one shilling wachana nayo.” akasema Sarai

Naibu huyo wa kitaifa wa chama cha United Democratic Alliance (UDA) alidai sera hiyo inayoshabikiwa na Bw Gachagua huenda ikaleta tofauti kubwa katika Chama tawala na uhasama mkubwa serikalini akisisitiza ni wazi sera hiyo itayatenga maeneo kame kimaendeleo.

“Kila wakati shares, sijui Mt.Kenya, sijui one shilling, one vote. Hii inaleta ukabila. Kauli kama hizi zinaweza lemaza maendeleo ya kitaifa. Inaleta ukabila, inaleta ubaguzi, inachangia hamasa miongoni mwa jamii. Wakati mwingine Rais au Naibu wake wakitaka kusema kauli kama hizi, kwanza wazungumze na sisi wawakilishi wa hizi jamii.”alisema Sarai

Wakati uo huo Hassan Omar alimtaka naibu huyo wa Rais kuwaleta wakenya pamoja pasi kutoa kauli zinazotishia kuvunja umoja na usawa wa wakenya akisema keki ya kitaifa ni ya kila mkenya wala si ya jamii fulani kwa msingi ya idadi ya watu wa jamii hiyo.

“Kama vile unainua kina mama na vijana unaweza pia kuinua jamii zilizotengwa. Hakuna ubaguzi kwa kuinua jamii zilizotengwa. Sisi tunataka kenya yenye umoja, tulete wakenya pamoja tuangalie namna nyingine ya kuleta usawa Hii mambo ya one man, one vote,one shilling wachana nayo sababu tukiendlea na hiyo story itakleta taharuki nchini”alisema Sarai.

Pingamizi sawia na za Sarai wali zilitolewa na seneta wa Tana River Danson Mungatana ambaye aliyesema watapinga sera ya sampuli hiyo akiongeza Kauli yake Naibu wa Rais inaakisi msimamo wake kama mtu binafsi wala sio msimamo wa serikali tawala ya Kenya Kwanza.

“Iwapo wewe ni mtu mwaminifu na mkweli, mbona hukuunga mkono mswada wa mabadiliko ya katiba wa BBI? Ni nini imebadirika sasa? Tumia nafasin yako kutatua changamoto zinazolikumba taifa, tumia mamalaka yako kujenga nchi ya kenya. Si kutumia nafasi yako kugawa wa kenya. Wakenya watapinga na kukataa pendekezo lolote la sampuli hiyo.Si kuanza kutupeleka katika siasa ambayo hatuelewi.Hatutakubali!” Alifoka Mungatana.

Kauli ya Mbunge huyo wa EALA inajiri baada ya Naibu wa Rais Riggy G kusema kuwa ataunga mkono mfumo wa ugavi wa mapato kwa msingi wa idadi ya watu ili kufikia kile alichodai kuwa ni usawa na haki Katika kaunti.

BY ISAIAH MUTHENGI