HabariNews

Utafiti Wabaini Ongezeko la Viwango vya Uhalifu Nchini Kutokana na Hali Ngumu ya Uchumi

Utafiti wa Kiuchumi wa mwaka 2023 umebainisha taswira mbaya ya hali ya usalama hapa nchini kwa ongezeko la asilimia 19 la visa vya uhalifu.

Utafiti huo uliofanywa na shirika la Takwimu za kitaifa la KNBS umebaini kuwa kuna visa vingi vya uhalifu vilivyoripotiwa kote nchini ambapo jumla ya kesi 104,842 ziliripotiwa.

Ongezeko hilo la uhalifu limelingana na kesi zilizoko mahakamani kukiwa na rekodi ya kesi 649,229 ambazo zingali kukamilishwa.

Aidha ripoti ya utafiti huo imeashiria ongezeko la idadi ya wafungwa gerezani kutoka wafungwa 169,000 mwaka 2022 hadi wafungwa 248,000 mwaka jana.

Wakati uo huo Serikali imebaini kupungua kwa idadi ya usajili wa wanaozaliwa na wanaofariki kote nchini, huku sekta ya elimu ikirekodi ongezeko la waliojiunga na taasisi za masomo katika viwango vyote vya elimu nchini Kenya.

BY MJOMBA RASHID