HabariNews

Kenya kuwa Mshirika mkuu asiye mwanachama wa jumuiya ya NATO

Rais wa Marekani Joe Biden anatarajiwa kulifanya taifa la Kenya kupewa heshima ya kuwa taifa mshirika mkuu asiye mwanachama wa Jumuiya ya NATO katika ziara ya siku nne ya rais William Ruto nchini Marekani.

Kenya itakuwa nchi ya kwanza kutoak eneo la Kusini mwa Sahara kutunukiwa hadhi hiyo hatua inayoashiria azma ya Marekani ya kuimarisha uhusiano Kenya ambayo kwa muda mrefu imekuwa na uhusiano na mataifa kamavile China na Urusi.

Hatua ya Biden kuitunuku Kenya hadhi hiyo inajiri wakati mipango ya kutumwa kwa vikosi vya kudumisha usalama nchini Haiti.

NATO ni jumuiya ya mataifa 32 ambayo yanashirikiana na kusadiana katika juhudi za kuimarisha miundo mbinu na mifumo ya ulinzi kama vifaa vya kivita mafunzo miongoni mwa mengine.

Kulingana na sheria ya kuundwa kwa muungano huo mataifa yanayopewa hadhi ya ushirika usio wa uanachama, hupata badhi ya manufaa kutoka kwa jumuiya hiyo hasa kutoka kwa mwanachama mkuu ambaye ni Marekani kama vile kupata mikopo ya utafiti wa mashirika na majaribio, kuwa kipaumbele kupata sialaha za ziada kutoka kwa wanachama na jumuiya ya NATO kwa ujumla  miongoni mwa faida nyingine.

Baadhi ya mataifa yaliyopata hadhi hiyo barani Afrika ni pamoja na Misri, Tunisia na Morocco.

BY EDITORIAL DESK