HabariNews

Viongozi wa kidini na wanaharakati wampongeza Gavana Nassir kwa kupiga Marufuku Muguka Kaunti ya Mombasa

Viongozi wa Kidini pamoja na wanaharakati wa kupambana na dawa za kulevya wameitaja hatua ya Gavana wa Kaunti ya Mombasa AbdulSwammad Shariff Nassir ya kupiga marufuku uingizaji wa Mogokaa Kaunti ya Mombasa kuwa muafaka.

Amina Abdallah ambaye ni Mwenyekiti wa Shirika la kuwatibu wagonjwa wa maradhi ya afya ya akili la Mombasa Women Network alisema mmea huo umekuwa kero katika jamii hasa kwa kuchangia maradhi ya akili.

Alisema wagonjwa wengi wa akili hasa miongoni mwa vijana walioletwa katika taasisi yake ya matibabu walikuwa wakila muguka.

‘Muguka ni mmea ambao umetupa dhiki sana Mombasa kwetu sisi leo tunasema ni sherehe kwa wale wagonjwa ambao tunawa discharge na nikajua kama wamepona kitu cha kunisikitisha ni kwamba baada ya muda mgonjwa yule nakutana naye njiani tayari ana ki pakiti cha mugukaa kwa hivyo ni kwamba hata tukiwatibu ni kama tunapoteza generation kwa njia moja ama nyingine’

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha kuwanasua waraibu wa dawa za kulevya cha Reach Out Centre Trust Taib AbdulRahman, anasema kwamba wameweka mikakati kabambe ya kuwatibu waraibu wa mogokaa.

‘Nikuangalia wale ambao wanapata athari kama hizi watapata njia gani mmbadala ya kuweza kurudi katika ile hali yao, kwa hivyo maono yetu, dhamira yetu ni moja kama gavana wetu na sisi tuko nyuma ya yeye ili kuangalia janga kama hili linaweza kupata njia nyingine’

BY EDITORIAL DESK

Comments (1)

  1. […] Viongozi wa kidini na wanaharakati wamempongeza Gavana Abdulswammad kwa kupiga… May 24, 2024 […]

Comments are closed.