HabariLifestyleNewsSiasa

JARIBIO LA KUMUUA RAIS WA MAREKANI LATIBUKA! HUKU MSHUKIWA MMOJA AKIUWAWA NA POLISI.

Maafisa wa polisi nchini marekani wamefanikiwa kumuua mtu mmoja huku watu wengine wawili wakijeruhiwa vibaya katika kile kilichotanjwa kuwa jaribio la kumuua aliyekuwa rais wan chi hiyo donald trump.

Picha kwa Hisani ya CNN

Kulingana na taarifa kutoka kitengo cha FBI ni kuwa trump yupo salama baada ya mtu mmoja kumyfytulia risasi iliyomkwaruza kwenye shavu na kumjeruhi kwenye sikio lake la kulia alipokuwa katika mkutano wa kufanya kampeni mjini Pennsylvania.

Hatahivyo rais wa marekani ameeleza kusikitishwa kwake kwa tukio hilo huku athibitisha kuwa trump anaendelea vizuri baada ya kuzungumza na madaktari wake na kuahidi uchunguzi wa haraka utaanzishwa na kueleza wananchi hatua zitakazochukuliwa.

“ Nnasikitika kuona jinsi watu walio na nia mbaya wanataka kuleta siasa mbaya hapa marekanai na mimi kam rais sitakubali. Nimeongea na madatari wanaomuhudumia trump na wameniambia kwasasa hali yake iko sawa.nitawapigia simu wakuu wa idara za usalama wote ili kupata ripoti kamili kuhusu tukio hilo “ asema rais wa marekani joe biden

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa x trump ameeleza kuwa yupo salama ila risasi hiyo ilimjeruhi sikio na kusababisha kutokwa na damu kabla ya kuanguka nyuma ya jukwaa na kupelekwa hospitali