HabariNews

KQ Yaelekeza Ndege za JKIA Kutua Mombasa na Tanzania kutokana na Hali mbaya ya Anga

Shirika la Ndege la Kenya Airways limelazimika kuelekeza ndege zilizokuwa zimepangiwa kutua uwanja wa JKIA leo hadi uwanja wa Moi mjini Mombasa na Kilimanjaro nchini Tanzania.

Hii ni kutokana na hali mbaya ya anga iliyopelekea kutoonekana vizuri kwa maeneo ya kutua ndege hizo jijini Nairobi.

Katika taarifa iliyotumwa mnamo Alhamisi Julai 25, KQ imeeleza kuwa abiria watarajie kucheleweshwa kwa safari zao  na kuwasili kwao jijini Nairobi lakikini ikawahakikishia mikakati yote inachukuliwa.

“We wish to inform our customers that we have this morning, diverted to Mombasa and Kilimanjaro some of our flights that were scheduled to land at JKIA.

This is due to poor visibility caused by poor weather conditions.” KQ ilieleza.

Vile vile ukaguzi wa moja kwa moja wa kufuatilia ratiba za ndege yaani Flight Radar 24 umeonyesha kuwa kuanzia mwendo was aa kumi na moja alfajiri, safari tisa za ndege zilielekezwa kutoka JKIA, nne zikiahirishwa na nne zikicheleweshwa.

 

BY MJOMBA RASHID